Psalms 18:2-50


2 a Bwana ni mwamba wangu,
ngome yangu na mwokozi wangu,
Mungu wangu ni mwamba,
ambaye kwake ninakimbilia.
Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu,
ngome yangu.
3 bNinamwita Bwana anayestahili kusifiwa,
nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

4 cKamba za mauti zilinizunguka,
mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
5 dKamba za kuzimu zilinizunguka,
mitego ya mauti ilinikabili.
6 eKatika shida yangu nalimwita Bwana,
nilimlilia Mungu wangu anisaidie.
Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu,
kilio changu kikafika mbele zake,
masikioni mwake.

7 fDunia ilitetemeka na kutikisika,
misingi ya milima ikatikisika,
vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.
8 gMoshi ukapanda kutoka puani mwake,
moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,
makaa ya moto yawakayo
yakatoka ndani mwake.
9 hAkazipasua mbingu akashuka chini,
mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
10 iAlipanda juu ya kerubi akaruka,
akapaa juu kwa mbawa za upepo.
11 jAlifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika,
hema lake kumzunguka,
mawingu meusi ya mvua ya angani.
12 kKutokana na mwanga wa uwepo wake
mawingu yalisogea,
ikanyesha mvua ya mawe
na umeme wa radi.
13 l Bwana alinguruma kutoka mbinguni,
sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
14 mAliipiga mishale yake na kutawanya adui,
naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.
15 nMabonde ya bahari yalifunuliwa,
na misingi ya dunia ikawa wazi
kwa kukaripia kwako, Ee Bwana,
kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.

16 oAlinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;
alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
17 pAliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,
kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
18 qWalinikabili siku ya msiba wangu,
lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
19 rAlinileta nje mahali penye nafasi tele,
akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

20 s Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
21 tKwa maana nimezishika njia za Bwana;
sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
22 uSheria zake zote zi mbele yangu,
wala sijayaacha maagizo yake.
23 vNimekuwa sina hatia mbele zake,
nami nimejilinda nisitende dhambi.
24 w Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.

25 xKwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu,
kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia.
26 yKwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu,
lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi.
27 zWewe huwaokoa wanyenyekevu,
lakini huwashusha wenye kiburi.
28 aaWewe, Ee Bwana, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka;
Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga.
29 abKwa msaada wako naweza kushinda jeshi,
nikiwa pamoja na Mungu wangu
nitaweza kuruka ukuta.

30 acKuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu,
neno la Bwana halina dosari.
Yeye ni ngao kwa wote
wanaokimbilia kwake.
31 adKwa maana ni nani aliye Mungu
zaidi ya Bwana?
Ni nani aliye Mwamba
isipokuwa Mungu wetu?
32 aeMungu ndiye anivikaye nguvu
na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.
33 afHuifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu,
huniwezesha kusimama mahali palipo juu.
34 agHuifundisha mikono yangu kupigana vita;
mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.
35 ahHunipa ngao yako ya ushindi,
nao mkono wako wa kuume hunitegemeza,
unajishusha chini ili kuniinua.
36 aiHuyapanua mapito yangu,
ili miguu yangu isiteleze.

37 ajNiliwafuatia adui zangu na nikawapata,
sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.
38 akNiliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena;
walianguka chini ya miguu yangu.
39 alUlinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita;
uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
40 amUliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia,
nami nikawaangamiza adui zangu.
41 anWalipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa;
walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.
42 aoNiliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo;
niliwamwaga nje kama tope barabarani.

43 apUmeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu;
umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa,
watu ambao sikuwajua wananitumikia.
44 aqMara wanisikiapo hunitii,
wageni hunyenyekea mbele yangu.
45 arWote wanalegea,
wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.

46 as Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu!
Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu!
47 atYeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi,
awatiishaye mataifa chini yangu,
48 auaniokoaye na adui zangu.
Uliniinua juu ya adui zangu;
uliniokoa toka kwa watu wajeuri.
49 avKwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee Bwana;
nitaliimbia sifa jina lako.
50 awHumpa mfalme wake ushindi mkuu,
huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake,
kwa Daudi na wazao wake milele.
Copyright information for SwhNEN